Blogger Widgets

February 20, 2013

Muonekano Mzima wa Ufunguzi wa Ofisi ya wema Sepetu Leo ndani ya Jiji la Dar Es Salaam


SI OFISI ya kitoto, ni ofisi ya bab kubwa iliyokwenda shule ikiwa imepambwa kwa fanicha na mashine za kisasa.
Naam hiyo ndio ofisi ya Wema Sepetu, mlimbwende na muigizaji nyota wa filamu, ni ofisi itakayobeba kazi zake za kila siku kupitia kampuni yake ya Endless Fame Film.
Akizungumza na waandishi wa wa habari masaa kadhaa yaliyopita wakati akiitambulisha rasmi kampuni yake, Wema Sepetu alisema Endless Fame Film itajishughulisha na utengenezaji wa filamu pamoja na kuandaa matamasha mbali mbali.
Ofisi za Wema Sepetu zitakazoanza kazi rasmi mwezi ujao zipo Mwananyamala koma koma, Dar es Salaam.Chanzo cha habari
Sehemu ya kumpuzika wageni

Mandhari ya ofisi kwa juu
Wema akiwa na Mama yake

Sehemu nyingine ya ofisi inavyoonekana


PICHA HIZI NI UFUNGUZI WA OFISI YA WEMA SEPETU HII LEO